Search This Blog

Translate

Monday, 30 May 2016

Nakupa Habari: AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO

Nakupa Habari: AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO: mathayo 7:21-23 (   21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba ...

AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO

mathayo 7:21-23 ( 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.)
Na je kwanini uishi tu bila utaratibu..?? eti tumeokololewa kwa Neema..? unaweza kutenda miujiza mingi...! kwa kutumia jina la kristo YESU lakini mwisho wako ni mauti ukipuuzia Haya...
AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO
1.      Ni lazima kutubu. (Luka 13:3,5; Mathayo 4:17)
2.      Ni lazima kuzaliwa mara ya pili. (Yohana 3:3; Yohana 14:15-17)
3.      Ni lazima tuwe wenye haki kuliko mafarisayo. (Mathayo 5:20; Yakobo 1:22)
4.      Tusifanye uovu. (Mathayo 13:40-43)
5.      Tusiwe watu waovu. (Mathayo 13:47-50)
6.      Ni lazima tusamehe. (Mathayo 6:14-15)
7.      Ni lazima tumpende YESU KRISTO kuliko mtu mwingine yeyote na kuliko maisha yetu. (Luka 14:26; Mathayo 28:19)