Search This Blog

Translate

Monday 30 May 2016

AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO

mathayo 7:21-23 ( 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.)
Na je kwanini uishi tu bila utaratibu..?? eti tumeokololewa kwa Neema..? unaweza kutenda miujiza mingi...! kwa kutumia jina la kristo YESU lakini mwisho wako ni mauti ukipuuzia Haya...
AMRI, SHERIA NA MAAGIZO YA BWANA YESU KRISTO
1.      Ni lazima kutubu. (Luka 13:3,5; Mathayo 4:17)
2.      Ni lazima kuzaliwa mara ya pili. (Yohana 3:3; Yohana 14:15-17)
3.      Ni lazima tuwe wenye haki kuliko mafarisayo. (Mathayo 5:20; Yakobo 1:22)
4.      Tusifanye uovu. (Mathayo 13:40-43)
5.      Tusiwe watu waovu. (Mathayo 13:47-50)
6.      Ni lazima tusamehe. (Mathayo 6:14-15)
7.      Ni lazima tumpende YESU KRISTO kuliko mtu mwingine yeyote na kuliko maisha yetu. (Luka 14:26; Mathayo 28:19)

8.      Ni lazima tujikane wenyewe, tujitwike msalaba wetu na kumfuata YESU KRISTO. (Mathayo 16:24)
9.      Hatupaswi kumkataa au kumkana YESU KRISTO. (Mathayo 10:32-33)
10.  Ni lazima tudumu katika IMANI. (Mathayo 10:22; 1wakor.15:1-2)
11.  Ni lazima tuzae matunda. (Yohana 15:2)
12.   Lazima tukae na kudumu ndani ya YESU KRISTO. (Yohana 15:6; )
13.  Lazima tuwe wanyenyekevu kama mtoto mdogo. (Luka 18:17; Mathayo 18:3)
14.  Lazima tufanye mapenzi ya Mungu. (Mathayo 7:21)
15.  Tusifanye watoto kutenda dhambi. (Mathayo 18:6-7)
16.  Tusiendelee kufanya dhambi. (Mathayo 18:8-9)
17.  Tusitamani (Mathayo 5:27-28, 1wakor. 6:9-10)
18.  Hatupaswi kuachana katika ndoa, isipokuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa uaminifu katika ndoa. (Mathayo 5:31-32)
19.  Hatupaswi kuwa na ndoa nyingine kama tumeachwa visivyostaili. (Mathayo 19:9)
20.  Hatupaswi kuwa watenda maovu au wasio fuata sheria yoyote. (7:22-23)
21.  Tusitumie maneno bila kujali. (Mathayo 12:37)
22.  Tusitake kuyaokoa maisha yetu. (Mathayo 16:25)
23.  Lazima tufanye mambo kwa kufuata njia za MUNGU. (Mathayo 22:13)
24.  Lazima tuwe atumishi waaminifu. (Mathayo 24:45-52)
25.  Lazima tuwe tayari kwa ajili ya kuja kwa Bwana. (Mathayo 25:10-13)
26.  Lazima tutumie talanta zetu vizuri. (Mathayo 25: 26-30)
27.  Tutahukumiwa kulingana na tuliyofanya. (Mathayo 25:41-43,46)
28.  Hatupaswi kumuonea YESU KRISTO aibu, wala maneno yake. (Marko 8:48)
29.  Lazima tuamini. (Marko 16: 15-16)
30.  Tusibweteke. (Luka 6:24-26)
31.  Lazima tumtii YESU KRISTO kama BWANA wetu (Luka 6:46; 2Wathesalonike 1:8-10)
32.  Wale wasiotii kwa makusudi wataadhibiwa vikali. (Luka 12:47-48; Waebrania 10:26)
33.  Lazima tupatanishwe na MUNGU. (Luka 12:58-59; Mathayo 18:34-35; Wakolosai 1:21-23)
34.  Ni lazima kufanya kila juhudi kupitia mlango ule mwembamba. (Luka 13:22-37)
35.  Lazima tuachane na kila kitu tulichonacho ili tuwe wanafunzi wa YESU KRISTO. (Luka 15:31-33)
36.  Lazima tuwe wenye kuaminika. (Luka 16:10-12; Mathayo 25:14-30; Luka 19:12-26)
37.  Tunapaswa kuwa waangalifu sana kuhusu hatari za utajiri. (Luka 6:24-26; ufunuo 3:15-18)
38.  Lazima tuwe waangalifu. (Luka 21:34-36)
39.  Lazima tumwamini yeye (YESU KRISTO). (Yohana 3:16-18)
40.  Lazima tumwamini MUNGU Baba. (Yohana 5:24; 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24; na 14:31). Kumuamini Baba ni kumtii Mwana.
41.  Lazima tumwamini Mwana-Bwana YESU KRISTO. (Yohana 5:36-40)
42.  Ni lazima tuamini kwamba YESU KRISTO ndiye kama alivyosema. (Yohana 8:24; 13:13; Mathayo 26: 63-64)
43.  Lazima tushike mafundisho ya YESU KRISTO. (Yohana 8:31-32)
44.  Lazima tushike neon la YESU KRISTO. (Yohana 8:51)
45.  Lazima tumkubali YESU KRISTO na maneno yake. (Yohana 12:48)
46.  Lazima tuje kwa Baba kwa njia ya YESU KRISTO. (Yohana 14:6-7)
47.  Ni lazima tumpende YESU KRISTO na kuyatii mafundisho yake. (Yohana 14:23-24; Waebrania 5:9)
48.  Ni lazima tudumu katika mzabibu na kuzaa matunda sana. (Yohana 15:5-8)

49.  Ni lazima tubakie na ladha yetu kama chumvi. (Mathayo 5:13; Waebrania 6:4-6; Warumi 1:5 na Mathayo 7:21)

No comments: