mathayo 7:21-23 ( 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.)
Na je kwanini uishi tu bila utaratibu..?? eti tumeokololewa kwa Neema..? unaweza kutenda miujiza mingi...! kwa kutumia jina la kristo YESU lakini mwisho wako ni mauti ukipuuzia Haya...
AMRI, SHERIA NA MAAGIZO
YA BWANA YESU KRISTO
1. Ni
lazima kutubu. (Luka 13:3,5; Mathayo 4:17)
2. Ni
lazima kuzaliwa mara ya pili. (Yohana 3:3; Yohana 14:15-17)
3. Ni
lazima tuwe wenye haki kuliko mafarisayo. (Mathayo 5:20; Yakobo 1:22)
4. Tusifanye
uovu. (Mathayo 13:40-43)
5. Tusiwe
watu waovu. (Mathayo 13:47-50)
6. Ni
lazima tusamehe. (Mathayo 6:14-15)
7. Ni
lazima tumpende YESU KRISTO kuliko mtu mwingine yeyote na kuliko maisha yetu.
(Luka 14:26; Mathayo 28:19)
8. Ni
lazima tujikane wenyewe, tujitwike msalaba wetu na kumfuata YESU KRISTO.
(Mathayo 16:24)
9. Hatupaswi
kumkataa au kumkana YESU KRISTO. (Mathayo 10:32-33)
10. Ni
lazima tudumu katika IMANI. (Mathayo 10:22; 1wakor.15:1-2)
11. Ni
lazima tuzae matunda. (Yohana 15:2)
12. Lazima tukae na kudumu ndani ya YESU KRISTO. (Yohana
15:6; )
13. Lazima
tuwe wanyenyekevu kama mtoto mdogo. (Luka 18:17; Mathayo 18:3)
14. Lazima
tufanye mapenzi ya Mungu. (Mathayo 7:21)
15. Tusifanye
watoto kutenda dhambi. (Mathayo 18:6-7)
16. Tusiendelee
kufanya dhambi. (Mathayo 18:8-9)
17. Tusitamani
(Mathayo 5:27-28, 1wakor. 6:9-10)
18. Hatupaswi
kuachana katika ndoa, isipokuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa uaminifu katika
ndoa. (Mathayo 5:31-32)
19. Hatupaswi
kuwa na ndoa nyingine kama tumeachwa visivyostaili. (Mathayo 19:9)
20. Hatupaswi
kuwa watenda maovu au wasio fuata sheria yoyote. (7:22-23)
21. Tusitumie
maneno bila kujali. (Mathayo 12:37)
22. Tusitake
kuyaokoa maisha yetu. (Mathayo 16:25)
23. Lazima
tufanye mambo kwa kufuata njia za MUNGU. (Mathayo 22:13)
24. Lazima
tuwe atumishi waaminifu. (Mathayo 24:45-52)
25. Lazima
tuwe tayari kwa ajili ya kuja kwa Bwana. (Mathayo 25:10-13)
26. Lazima
tutumie talanta zetu vizuri. (Mathayo 25: 26-30)
27. Tutahukumiwa
kulingana na tuliyofanya. (Mathayo 25:41-43,46)
28. Hatupaswi
kumuonea YESU KRISTO aibu, wala maneno yake. (Marko 8:48)
29. Lazima
tuamini. (Marko 16: 15-16)
30. Tusibweteke.
(Luka 6:24-26)
31. Lazima
tumtii YESU KRISTO kama BWANA wetu (Luka 6:46; 2Wathesalonike 1:8-10)
32. Wale
wasiotii kwa makusudi wataadhibiwa vikali. (Luka 12:47-48; Waebrania 10:26)
33. Lazima
tupatanishwe na MUNGU. (Luka 12:58-59; Mathayo 18:34-35; Wakolosai 1:21-23)
34. Ni
lazima kufanya kila juhudi kupitia mlango ule mwembamba. (Luka 13:22-37)
35. Lazima
tuachane na kila kitu tulichonacho ili tuwe wanafunzi wa YESU KRISTO. (Luka
15:31-33)
36. Lazima
tuwe wenye kuaminika. (Luka 16:10-12; Mathayo 25:14-30; Luka 19:12-26)
37. Tunapaswa
kuwa waangalifu sana kuhusu hatari za utajiri. (Luka 6:24-26; ufunuo 3:15-18)
38. Lazima
tuwe waangalifu. (Luka 21:34-36)
39. Lazima
tumwamini yeye (YESU KRISTO). (Yohana 3:16-18)
40. Lazima
tumwamini MUNGU Baba. (Yohana 5:24; 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24; na 14:31). Kumuamini
Baba ni kumtii Mwana.
41. Lazima
tumwamini Mwana-Bwana YESU KRISTO. (Yohana 5:36-40)
42. Ni
lazima tuamini kwamba YESU KRISTO ndiye kama alivyosema. (Yohana 8:24; 13:13;
Mathayo 26: 63-64)
43. Lazima
tushike mafundisho ya YESU KRISTO. (Yohana 8:31-32)
44. Lazima
tushike neon la YESU KRISTO. (Yohana 8:51)
45. Lazima
tumkubali YESU KRISTO na maneno yake. (Yohana 12:48)
46. Lazima
tuje kwa Baba kwa njia ya YESU KRISTO. (Yohana 14:6-7)
47. Ni
lazima tumpende YESU KRISTO na kuyatii mafundisho yake. (Yohana 14:23-24;
Waebrania 5:9)
48. Ni
lazima tudumu katika mzabibu na kuzaa matunda sana. (Yohana 15:5-8)
49. Ni
lazima tubakie na ladha yetu kama chumvi. (Mathayo 5:13; Waebrania 6:4-6;
Warumi 1:5 na Mathayo 7:21)
No comments:
Post a Comment